Hayo yanajiri katika hali ambayo Rais Francois Hollande wa Ufaransa amesema endapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litaunga mkono, upo uwezekano wa kuingilia kijeshi mgogoro wa Syria. Hollande, ambaye kesho Ijumaa anatazamiwa kukuktana na kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Russia huko mjini Paris amesema ataendelea kuishawishi Moscow iunge mkono maazimio ya Baraza la Usalama dhidi ya Syria. Sambamba na hayo, na katika hatua iliyochukuliwa kwa uratibu ili kuzidisha mashinikizo dhidi ya serikali ya Damascus, mabalozi wa Syria wametimuliwa kwa mpigo katika nchi za Marekani, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani. Japokuwa mauaji ya mamia ya raia katika mji wa Houla huko magharibi mwa Syria yametumiwa na madola ya Magharibi kuwa kisingizio cha kushadidisha mbinyo dhidi ya Syria, lakini Russia naChina zingali zinashikilia msimamo wao wa kupinga uingiliaji wowote wa kijeshi nchini humo kwa kutumia idhini na baraka za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pamoja na hayo nchi za Magharaibi zinaendelea kuzishawishi Moscow na Beijing ziunge mkono maazimio ya Baraza la Usalama dhidi ya Syria. Katika muelekeo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague, siku ya Jumatatu alielekea Russia kwa ajili ya mazungumzo na mashauriano na mwenzake wa nchi hiyo Sergei Lavrov. Kabla ya hapo Tom Donilon, mshauri wa Usalama wa Taifa wa Rais wa Marekani alifanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Russia juu ya mpango wa Washington wa upokezanaji madaraka nchini Syria. Mpango huo unaotaka kufuata kigezo kilichotumika nchini Yemen ulijadiliwa hapo kabla na Rais Barack Obama wa Marekani na Waziri Mkuu wa Russia Dmitri Medvedev pambizoni kwa kikao cha kundi la G8. Russia inaitakidi kuwa muelekeo wa upande mmoja wa nchi za Magharibi unaotosheka na kulaani upande mmoja tu kati ya pande mbili hasimu katika mgogoro wa Syria ni kizuizi cha kumaliza mgogoro wa nchi hiyo. Na ndiyo maana inaendelea kuunga mkono mpango wa vipengele sita wa Kofi Annan na kutaka mgogoro wa Syria uhatimishwe kwa kuzingatia mpango huo. Pamoja na kwamba mpango huo haujafikia kwenye mkwamo lakini Magharibi na waitifaki wao katika eneo wangali wanapigia upatu wazo la kuingilia kijeshi nchini Syria, suala ambalo kwa mtazamo wa Naibu wa kwanza wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Andrey Denisov lina utashi na malengo ya kisiasa.
Thursday, May 31, 2012
Juhudi za kukabiliana na mpango wa Magharibi wa kutaka kuingilia kijeshi Syria

Posted by
AO Secretarial & Technology Supplies
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment