Watu kadhaa wameuawa baada ya ndege zisizo na rubani za Marekani
kushambulia kwa makombora maeneo ya nje ya mji mkuu wa Somalia
Mogadishu.Hujuma hiyo Jumanne usiku ya ndege za kigaidi za Marekani
zisizo na rubani imelenga maeneo kadhaa kusini mwa Mogadishu. Wakati huo
huo ndege moja isiyo na rubani ya Marekani imeanguka karibu na kituo
cha kijeshi cha Halane kusini mwa Mogadishu.Maafisa wa Somalia wamethibitisha kuwa ndege hiyo ya kijasusi ilianguka siku ya Jumatano.
Oktoba
28 mwaka jana Marekani ilikiri kushambulia Somalia kwa ndege zake hizo
kutumia kituo cha kijeshi cha siri kilichoko Ethiopia, eti kwa lengo la
kukabiliana na waasi wa as Shabab.
Hata hivyo raia na watu wa kawaida Somalia ndio wahanga wakuu wa mashambulizi ya ndege za kigaidi za Marekani nchini humo.
www.kiswahili.irib.ir






No comments:
Post a Comment