Kiongozi wa upinzani wa Malawi Peter
Muatharika leo ameapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo baada ya Joyce
Banda kushindwa katika uchaguzi wa rais uliozusha mjadala.
Rais huyo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya
Nje wa Malawi na kaka wa rais wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo aliyefariki
dunia Bingu Wa Muatharika, amekula kiapo leo mbele ya mahakama kuu ya
nchi hiyo katika mji wa Blantyre.
Katika hotuba yake ya kwanza baada ya
kuapishwa, Peter Mutharika amekiri kuwa Malawi inakabiliwa na matatizo,
lakini akataka washirikiane pamoja ili kuijenga nchi hiyo ambayo
inaelekea kuanguka. Rais anayeachia ngazi Joyce Banda aliyeshindwa
katika uchaguzi, hatimaye mapema leo alikubali matokeo na kumpongeza
Mutharika kwa kushinda. Baada ya uchaguzi Bi. Banda alidai kumetokea
uchakachuaji na kuamuru uchaguzi ufutwe, suala ambalo halikuafikiwa na
mahakama kuu ya Malawi.
No comments:
Post a Comment