Shirika la Msamaha Duniani Amnesty
International limewakosoa maafisa wa India kutokana na ubaguzi na
unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana unaoshuhudiwa
nchini humo. Shirika hilo limeitaka serikali ya India kuchukua hatua za
haraka za kulinda haki za wanawake na kuacha kuwasamehe wanaotenda
jinai hizo.
Pia Amnesty International imewataka maafisa wa India
kuchunguza bila upendeleo tukio la hivi karibuni la kubakwa na kuuawa
wasichana wawili katika kijiji cha jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh.
Ripoti zinasema kuwa, katika kila dakika
22 mwanamke mmoja hubakwa nchini India. Mwaka jana serikali ya nchi
hiyo ilitangaza adhabu ya kifo kwa watakaobaka kwa pamoja hata kama
atakayebakwa atabakia hai. Adhabu hiyo ilitangazwa, baada ya msichana wa
chuo kikuu aliyekuwa na miaka 23 kubakwa na kundi la wanaume na kisha
kurushwa nje ya basi katika tukio la kinyama lililofanywa katika mji
mkuu New Delhi mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment