Nchi za Kiarabu zilizoko katika eneo la Ghuba ya Uajemi zimeendeleza
uadui dhidi ya Mashia wa Lebanon, baada ya serikali ya Qatar kuwafukuza
nchini humo raia 17 wa Lebanon kwa tuhuma wanashirikiana na Harakati ya
Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon. Taarifa zinasema
kuwa, serikali za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu nazo hivi
karibuni zilitangaza kuwafukuza raia kadhaa wa Lebanon kwa tuhuma za
kushirikiana na harakati ya Hizbullah. Televisheni ya Qatar imeeleza
kuwa, harakati ya Hizbullah ilikuwa na nafasi kubwa katika shambulio
lililofanywa na majeshi ya Syria na hatimaye kuukomboa mji wa
kiistratijia wa Qusayr mwanzoni mwa mwezi huu.
Hii ni katika hali
ambayo, serikali za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi zimekuwa
zikishindwa kuficha hasira na chuki zao dhidi ya mafanikio ya wapiganaji
wa Hizbullah katika mapambano yao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa
Israel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment