Mahakama ya Stockholm nchini Sweden imemuhukumu adhabu ya kifungo cha
maisha jela Stanislas Mbanenande Mswidi mwenye asili ya Rwanda baada ya
kupatikana na hatia ya kushiriki kwenye mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
Mahakama hiyo imeeleza, Mbanenande akishirikiana na watu wengine
alitenda jinai za mauaji ya halaiki nchini humo katika eneo la Kibuye
magharibi mwa Rwanda kuanzia tarehe 6 Aprili hadi 30 Juni mwaka 1994.
Hata hivyo, wakati wa kusikilizwa kesi hiyo, Stanislas alikadhibisha
tuhuma hizo zilizoelekezwa dhidi yake.
Mashuhuda kadhaa wameeleza
mahakamani hapo kwamba, Mbanenande alishiriki kikamilifu kwenye vitendo
vya mauaji na hasa kwenye kanisa moja na uwanja wa michezo nchini
Rwanda. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Stanislas Mbanenande alikimbilia
nchini Sweden mwaka 2007, na mwaka uliofuata alipata uraia wa nchi hiyo.
Imeelezwa kuwa, watu wasiopungua laki nane waliuawa kwenye machafuko ya
Rwanda mwaka 1994.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment