Muhammad Morsi, mgombea wa Ikhwanul Muslimin katika uchaguzi wa rais Misri.
Huku zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi wa Rais wa Misri likielekea ukingoni, matokeo yanaonesha kuwa hadi sasa mgombea wa harakati ya Ikhwanul Muslimn anaongoza katika uchaguzi huo.
Kundi la Ikhwanul Muslimin limetangaza kwamba baada ya kuhesabiwa asilimia 90 ya kura katika mikoa tofauti ya Misri, Muhammad Morsi mgombea wa chama cha Usawa na Uadilifu ambacho ni tawi la kisiasa la harakati hiyo anaongoza kwenye kinyang'anyiro hicho.
Matokeo hayo pia yanaonyesha kwamba Ahmed Shafiq, Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa dikteta Hosni Mubarak uliopinduliwa na wananchi nchini humo anashika nafasi ya pili na wagombea wengine wakifuata nyuma.
Wagombea hao wawili ndio wanaotarajiwa kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa Rais wa Misri utakaofanyika tarehe 16 na 17 mwezi ujao wa Juni.

No comments:
Post a Comment