
Hatua hiyo inahesabiwa kuwa pigo kubwa kwa wanamgambo hao waliokuwa wakitumia mji huo kushambulia mji mkuu Mogadishu.
Paddy Ankunda, msemaji wa kikosi cha AMISON amesema kwamba, wamevuuka mto Shabelle na hivi sasa wako katika mji wa Afgoye ambao tayari wanaudhibiti. Amesema, wamekuwa wakipigana tangu Jumanne na hivi sasa wamefanikiwa kufikia lengo walilokusudia.
Ankunda aidha ameongeza kuwa, wapiganaji wa ash Shabab wanaendelea kuukimbia mji huo kuelekea maporini na kwamba vikosi vya AU hivi sasa vimeimarisha usalama katika barabara za kuingia kwenye mji wa Afgoye, ambazo ni njia kuu ya kutoka kusini mwa Somalia kuelekea mji mkuu Mogadishu.
No comments:
Post a Comment