Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, May 26, 2012

Kamishna wa Haki za Binadamu awataka Wamagharibi kuiondolea vikwazo Zimbabwe


Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, amezitaka nchi za Magharibi ziiondolee Zimbabwe vikwazo.
Navi Pillay amesema kuwa, nchi za Magharibi zinapaswa kuiondolea Zimbabwe vikwazo ili kusaidia kufanyika uchaguzi wa nchi hiyo kwa uhuru na katika katika mazingira mazuri.
Aidha amesisitiza kuwa, kambi za kisiasa nchini Zimbabwe bado hazijajulikana vizuri na kwamba kuna uwezekano wa kutokea machafuko katika uchaguzi ujao wa nchi hiyo.
Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa aidha amesisitiza kuwa, nchi za Magharibi zinapaswa kuiondolea serikali ya Harare vikwazo kwa uchache hadi wakati wa kufanyika uchaguzi nchini humo.

No comments: