Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, May 26, 2012

IAEA: Iran haijakengeuka sheria katika miradi yake ya nyuklia


Amano
Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, Yukiya Amano, ametoa ripoti mpya iliyosisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, hakujashuhudiwa ukengeukaji wa sheria katika mipango ya nyuklia ya Iran.
Ripoti hiyo mpya ya Amano iliyotolewa jana Ijumaa imewasilishwa kwa Bodi ya Magavana ya wakala wa IAEA.
Kwa upande wake, Ali Asghar Sultaniyeh, Mwakilishi wa Iran katika wakala wa IAEA amesema kwamba, ripoti hiyo mpya ya Amano ni ushahidi mwingine unaonesha kuwa mipango ya nyuklia ya Iran ni ya amani na pia ni mafanikiko katika uwanja wa teknolojia ya atomiki hasa urutubishaji urani na ushirikiano ulionyeshwa na Iran kwa wakala huo.
Ripoti hiyo itajadiliwa katika mkutano ujao wa Bodi ya Magavana ya IAEA utakaofanyika tarehe 4 Juni mjini Vienna Austria.

No comments: