Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyalaumu makundi ya kigaidi nchini Syria kwa kuendeleza machafuko na kusema kwamba inaonesha kuwa milipuko inayotokea nchini humo inafanywa na megenge hayo ya kigaidi.
Ban aidha amesema, kumekuwepo na mafanikio lakini si ya kutosha katika utekelezwaji wa mpango wa vipengee 6 wa Kofi Annan, mpatanishi wa wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Arab League katika mgogoro wa Syria.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aidha ameitaka serikali ya Damascus kuendelea kutekeleza ahadi yake ya kusitisha mapigano, kuondoa silaha nzito na vikosi vya kijeshi katika miji yenye raia wengi, kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wahitaji na kuheshimu haki za binadamu.
Pia ameyataka makundi ya upinzani ya Syria kukomesha vitendo vyao vya kigaidi na kuheshimu haki za binadamu.
Aidha amesema kuwepo wasimamizi 271 wa Umoja wa Mataifa wasio na silaha wanaosimamia amani nchini Syria kumesaidia kutuliza hali ya mambo nchini humo.

No comments:
Post a Comment