skip to main |
skip to sidebar
Baghdadi al-Mahmudi : Niko tayari nikashitakiwe kwengineko na si Libya
Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa zamani wa Libya wa dikteta aliyeng'olewa madarakani Muammar Gaddafi ameeleza kusikitishwa na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Tunisia ya kumkabidhi kwa serikali ya Libya. Baghdadi al-Mahmudi ameielezea hatua hiyo kuwa ni kutoa moja kwa moja hukumu ya kifo dhidi yake. Akizungumzia kupinga vikali hatua hiyo sambamba na kukosoa uwezo wa serikali ya mpito nchini ya Libya ya kuunda mahakama ya uadilifu, Al-Mahmudi amesema, katika kipindi hiki kifupi haifai kutarajiwa kuundwa mahakama ya kiuadilifu hata kama itakuwa na sifa duni kabisa za Kimataifa. Aidha Baghdadi al-Mahmudi amepinga vikali kuhudhuria katika mahakama za Libya na kuongeza kuwa, nchi yoyote au utawala wowote ambao utakuwa na mahakama ya kiuadilifu basi yeye yuko tayari kwenda kujibu tuhuma dhidi yake na sio Libya.
No comments:
Post a Comment